Linda: Simameni kidete kulinda na kutetea Injili ya uhai!

Mtumishi wa Mungu Paskal Linda anasema, kumekuwepo na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ya tiba ya mwanadamu ambayo kwa sasa inatishia Injili ya uhai; kwa kusababisha kinzani katika kanuni maadili, kijamii na kisheria, kiasi hata cha kutishia utu na heshima ya binadamu mintarafu nadharia na vitendo vya sayansi. 


Kanisa kwa upandwe wake linapenda kujikita katika asili, umuhimu na hatima ya maisha ya binadamu ili kufafanua mambo yanayotishia uhai wa binadamu; ubora wa maisha pamoja na kuangalia fursa zinazotolewa na sayansi pamoja na teknolojia katika matamanio halali ya maboresho ya maisha ya binadamu bila kutumbukizwa katika mtego wa wajanja wachache kutaka faida kubwa kwa ajili ya mafao yao binafsi.


Licha ya maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia duniani, lakini bado kuna umaskini mkubwa wa hali na kipato duniani, changamoto kwa watunga sera na maendeleo ya binadamu kutoa kipaumbele cha kwanza kwa binadamu. Paskal Linda anawaalika waamini kuwa kweli ni mashuhuda wa Injili ya uhai na furaha ya kweli dhidi ya utamaduni wa kifo! Hii ni dhamana inayowataka kuwajibika, kupenda kwa dhati na kuwaheshimu watu katika hatua zao mbali mbali za maisha! Changamoto hii inatekelezwa na Mama Kanisa kwa kujikita katika mwanga wa Neno la Mungu unaofumbata kazi ya Uumbaji na Ukombozi, kielelezo makini cha baraka na upendo wa Mungu kwa binadamu wote ambao Mwenyezi Mungu ameamua kufunga nao Agano katika kazi ya uumbaji na historia katika ujumla wake.
Idhaa ya Kiswahili ya Linda HABARI.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

St. Bruno

Prayer of the Day for Wednesday, October 25